MJUMBE wa timu ya kampeni ya CCM, Dk Harrison Mwakyembe, amesema sakata la kashfa ya Richmond, haliwezi kuachwa kuzungumzwa na wanaCCM kwa kuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ameanza kusingizia watu wengine kuhusika na kashfa hiyo, jambo ambalo alisema haliwezi kuachwa lipotee bila kujibiwa.
Aliyasema
hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Ubungo jana, mkutano uliokwenda
sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dk
Didas Massaburi.
“Unaposema kuna wakubwa juu waliamuru Mkataba wa Richmond usivunjwe maana yake unamsema Rais wa nchi.
“Unaposema kuna wakubwa juu waliamuru Mkataba wa Richmond usivunjwe maana yake unamsema Rais wa nchi.
"Katika
suala lile hakuna rais wala nani, mhusika mkuu ni Lowassa na alifanya
hivyo kwa uroho tu wa kutaka kujipatia fedha na upo ushahidi wa maboksi
mawili.
“Tulimpa masharti mawili; Kwanza ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana wa yeye kushiriki. Pili ilikuwa ni kwa Bunge kuthibitisha ushiriki wake endapo angegoma.
“Tulimpa masharti mawili; Kwanza ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana wa yeye kushiriki. Pili ilikuwa ni kwa Bunge kuthibitisha ushiriki wake endapo angegoma.
"Alichofanya ni kuamua kujiuzulu ili kukwepa aibu. Sasa katika hili rais anatokea wapi au anaposema alionewa ni katika lipi?” Alihoji.
Akizungumzia kutofuatana na Dk Magufuli katika mikutano yake kuzungumzia kashfa ya Richmond na kuachia makada wengine kuzungumzia suala hilo, Dk Mwakyembe alisema ni kutokana na wajumbe 32 wa Kamati ya Kampeni kuwa na majukumu katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wale
wajumbe 32 tumegawanyika katika maeneo mbalimbali, na kila mtu anaonana
na wananchi kwa njia na staili tofauti lakini lengo likiwa ni
kuhakikisha kuwa CCM inaibuka na ushindi wa kishindo. Hata kama wajumbe
wote 32 tukifuatana na Dk Magufuli hatuwezi kuzungumza wote kutokana na
muda,” alisema.
Akimnadi
Dk Masaburi, Dk Mwakyembe ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la
Kyela na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema mgombea huyo
wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM ni aina ya wachapakazi
ambao wanahitajika katika uongozi ujao wa Dk Magufuli katika kuwaletea
wananchi maendeleo.
“Jimbo
la Ubungo ni jimbo la kimkakati kutokana na umuhimu wake. Kwanza ni
Jimbo la viwanda, pili ni lango la Jiji na hivyo ni sura ya Dar es
Salaam, lakini tatu ni Jimbo la Elimu ya Juu kutokana na kuwepo kwa Chuo
Kikuu na Chuo cha Usafirishaji. Dk Masaburi ni aina ya mbunge
anayehitajika kuliongoza ili kulifanya Taifa kulitendea haki,” alisema.