Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira.
Dk
Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele
hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha
kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za
uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi
hizo lakini wana uwezo wa kuongoza.
Katika
kampeni zake mjini Iringa jana, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali
yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo
la ajira kwa vijana.
Alisema
kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa
kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo
inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo.
‘’Vijana
wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana
na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo
atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa?.. tena wanataka uzoefu wa miaka
mitano huo uzoefu wataupata wapi, nataka kama kuna uwezekano haya mambo
ya uzoefu yafutwe kabisa,” Dk magufuli.
Alieleza
kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda ili kumaliza
tatizo hilo sugu kwa wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla.
Aliwataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.
Aliwataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.