Mkutano wa LOWASSA Jana Ulivunjika mkoani Tanga baada ya Umati mkubwa wa watu Kujitokeza na Kuzimia kwa wingi - LEKULE

Breaking

29 Sept 2015

Mkutano wa LOWASSA Jana Ulivunjika mkoani Tanga baada ya Umati mkubwa wa watu Kujitokeza na Kuzimia kwa wingi

Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa jana  alilazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga
 
Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8  zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo  kwa  sababu  watu  walianza  kuzimia  kwa  kasi
Akina  mama, watoto  wakipatiwa  huduma  ya  kwanza  baada  ya  kuzimia
Watu  wakiwa  wamezimia  baada  ya  kukosa  hewa
Gharika  la  Lowassa