WAKATI Waislamu kote duniani wakiwa katika simanzi kuu kutokana na vifo vya mahujaji zaidi ya 700 katika mji mtakatifu wa Makka, Saudia Arabia, imethibitika kuwa zaidi ya mahujaji 50 wa Tanzania, hawajulikani walipo.
Aidha,
idadi ya mahujaji wa Tanzania waliokufa katika tukio la kukanyangana
katika mji huo mtakatifu, imefikia watano, baada ya mtu mmoja zaidi
kuthibitika kufa na mwingine kupatikana akiwa majeruhi.
Kutokana
na ongezeko hilo la vifo, idadi ya Watanzania waliokufa wakiwa katika
ibada ya Hijja, moja ya nguzo kuu ya Kiislamu, sasa imefikia watu
watano. Hayo yamethibitishwa jana na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakari
Zuberi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoituma akiwa Makka.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa “Bakwata
kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia, tumepata taarifa
kwamba maiti mmoja amepatikana, ametambulika kwa jina la Shafi Khamisi
Ali. Pia Nasra Nassor Abdallah amepatikana akiwa amepata majeraha.
Mwenyezi Mungu atawapa tahfif Insha Allah.
“Kadhalika
tumepokea taarifa ya kutopatikana kwa Watanzania 50 ambao walikuwapo
Makka wakati wa tukio hilo. Kati yao 30 walisafiri kupitia taasisi ya
Ahlu Daawa, taasisi ya Khidma watu 17 na TCDO watu watatu.”
Taarifa
ya Mufti Zuberi imekuja ikiwa ni mwendelezo wa taarifa juu ya tukio la
kuhuzunisha, lililotokea wiki iliyopita huko Mina, Saudi Arabia, ambako
mahujaji zaidi ya 700 walikufa na wengine kujeruhiwa wakati wakielekea
kwenye Jamaraat, ambapo palitokea msongamano mkubwa.
Alisema
anatambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa, ambazo zinazidisha taharuki
kwa ndugu na jamaa wa mahujaji. Hata hivyo, aliwaomba Waislamu kuwa na
moyo wa subira, kwani juhudi za kuwatafuta mahujaji wengine zinaendelea.
Aliwaombea
dua wale waliotangulia mbele ya haki na Mwenyezi Mungu, apokee ibada
zao, awasamehe madhambi yao na awakusanye katika kundi la waja wema
peponi.
“Kutokana na mtihani huu kwetu sote, nawaombea dua wafiwa Mola awape subra na ustahmilivu na kuwaombea wagonjwa wapate tahfif.Pia nawaomba Waislamu wote Tanzania kuwaombea dua waathirika wa mtihani huu.
“Mwisho nichukue fursa hii kuwaomba wale wote wenye nafasi ya kuwafariji na kuwasaidia wanafamilia, ambao katika ajali hii wameondokewa na nguzo katika familia hizo wafanye hivyo.
"Tuwasaidie wanafamilia hawa kwa hali na mali katika wakati huu mzito sana kwao ili tuwapunguzie majonzi na unyonge walionao,” ilisema taarifa hiyo ya Mufti.