Masanga Said Bori, anayevuja damu.
Boniphace Ngumije na Mayasa Mariwata
BALAA! Mkazi wa
Mtaa wa Manyoni, Ilala jijini Dar aliyejulikana kwa jina la Masanga
Said Bori (pichani), Jumamosi iliyopita nusura atolewe uhai akitetea
mirathi ya nyumba iliyoachwa na shangazi yake, Mwanafatima binti Mchinga
akiwa na ndugu zake, Panya Bori, Mchinga Bori, Mwanafatima Bori na
Zaujiha Bori.
Kwa mujibu wa chanzo, nyumba hiyo namba 27/1 yenye mirathi namba 79/2006 waliyorithishwa ndugu hao na shangazi yao ambaye ni marehemu, alipewa kusimamia mzee mmoja aitwaye Said Athuman Kingo akiwa ni mmoja wa familia hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo, nyumba hiyo namba 27/1 yenye mirathi namba 79/2006 waliyorithishwa ndugu hao na shangazi yao ambaye ni marehemu, alipewa kusimamia mzee mmoja aitwaye Said Athuman Kingo akiwa ni mmoja wa familia hiyo.
“Muda mfupi tangu shangazi yao afariki
dunia, Masanga alionekana kutoelewana na ndugu zake kwa sababu alikuwa
anapangisha baadhi ya vyumba bila kuwashirikisha jambo lililowafanya
wafikishane Mahakama ya Mwanzo Ilala ambapo baada ya shauri lao
kusikilizwa, iliamriwa nyumba hiyo iuzwe ili wagawane pesa.
Sintofahamu ikiendelea eneo la tukio.
“Wakatafuta mteja, wakampata kwa
shilingi milioni mia moja, Masanga akakataa nyumba hiyo kuuzwa kwa kiasi
hicho akidai thamani yake ni kubwa, akataka iuzwe kwa shilingi milioni
160. Mahakama ikampa yeye muda wa wiki tatu kutafuta mteja lakini
hakuweza kumpata,” kilisema chanzo.
…Wakiamuliwa.
Kikaendelea: “Masanga alipomkosa mteja
baada ya muda huo kupita mahakama ilitoa ridhaa ya nyumba kuuzwa kwa
kiasi cha shilingi milioni 100, jambo lililofanyika na baada ya hapo
warithi wakagawana shilingi milioni 24 kila mmoja huku pesa za Masanga
zikienda kuhifadhiwa kwenye mfuko wa hifadhi wa mahakama.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakifika eneo la tukio kutuliza ghasia.
“Masanga hakwenda kuchukua pesa zake
badala yake akarudi mahakamani na kutaka shauri hilo libadilishwe lakini
haikuwezekana. Mahakama ikatoa ridhaa kwa wanunuzi wa nyumba hiyo,
Zulfa Jumanne Ileswa na Mwajuma Jumanne Ileswa wamtoe kwa nguvu kwa
kutumia Kampuni ya Madalali ya Rimina ambao walikwenda kuifanya kazi
hiyo sanjari na kuibomoa.
“Lakini
baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kufika kwenye nyumba hiyo, Masanga
hakukubali nyumba ibomolewe jambo lililozua timbwili zito na mtaa
kufungwa kwa wingi wa watu na fujo.
“Huwezi
amini, Masanga alitoka ndani na panga kupambana na wafanyakazi wa
Rimina lakini ile anataka kumkata baunsa wa kampuni hiyo, alikwepa na
kumnyang’anya kisha kumkata nalo yeye kichwani. Damu zilianza kumwagika
chapachapa.”
Kwa
mujibu wa shuhuda huyo, baada ya hapo hali ya amani ilivurugika jambo
lililofanya wasamaria wema kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Ilala ambapo
askari walifika na kutokana na vurugu zilizokuwepo walipiga mabomu ya
machozi na kuzuia nyumba hiyo kuendelea kuvunjwa.
Wakamchukua Masanga na wafanyakazi wa
Kampuni ya Rimina na kwenda nao kituoni kwa ajili ya mahojiano zaidi juu
ya kilichokuwa kinaendelea.
No comments:
Post a Comment