Mgombea udiwani wa Kata ya Kilakala kwa tiketi ya Chadema , Mapunda Lusewe akitambulisha familia yake jukwaani.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
MGOMBEA udiwani
wa Kata ya Kilakala kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kwa baraka za muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Mapunda Lusewe, Jumamosi iliyopita alizindua kampeni kwa kuibua
minongo’no kufuatia kitendo chake cha kutumia muda mrefu kutambulisha
familia yake jukwaani.
…Akimtambulisha mwanaye.
Lusewe alipanda jukwani sambamba na
familia yake ya watu watano na yeye mwenyewe wa sita ambapo ni watoto
wake wanne, akiwemo mmoja wa miezi tisa na mke.
…Akimtambulisha mkewe.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi
waliouhudhuria mkutano huo walionekana kupinga kitendo cha mgombea huyo
kwa kushirikiana na mkewe, Herieth Fungo kumtoa mtoto huyo mchanga na
kumnadi jukwaani majira ya saa 12 kasoro jioni ambapo baridi kali
ilivuma kutoka Milima ya Uluguru iliyopo jirani kabisa na eneo hilo la
mkutano.
“Hii
jamani si haki. Kwanza ametumia muda mrefu kutambulisha watoto wake…
yaani muda wa kunadi sera yeye anashughulika na familia yake jukwaani,”
alisema mtu mmoja bila kutaja jina lake.
Akaendelea:
“Halafu si mbaya mgombea kupandisha familia jukwaani, hata Rais Obama
(wa Marekani) aliwahi kufanya hivyo. Lakini si kutumia muda mrefu.
“Kingine ni yule mtoto. Unajua ni saa
kumi na mbili kasoro sasa. Baridi ya Milima ya Uluguru yote inamwingia,
wangeangalia na hilo.”
Pamoja na yote, mgombea huyo alisema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo ataleta maendeleo huku wananchi wakimshangilia.
No comments:
Post a Comment