Moja
kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na
mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi
miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa
ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.
NA K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi
miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo
unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash,
alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa
wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika
kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za
kampuni kuwajibika kusaidia jamii.
” Alisema
” Alisema
“Ninayo
furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya
shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka
huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua
Akitoa
mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani
Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu
wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000,
kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji
kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na
ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu
shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi
mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9),
Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa
na gharama ya shilingi 174,392,000.
Hali
kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na
Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi
256,154,706.
Akitoa
shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya
alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia
jamii inayozunguka mgodi huo.
“Nataka
niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano
mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale
wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na
maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa
kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki
mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.
Kaimu
Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu,
BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya
Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima
kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko
Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi
mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya
shilingi Bilioni 1.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu
wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga,
Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi,
Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu,
zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na
kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri
ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi
Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015.
No comments:
Post a Comment