Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza siku ya Jumanne,
wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio
linalowasilisha kwa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali Malengo na
Ajenda mpya za Maendeleo Endelevu ( Ajenda 2030) Anaonekana pia Rais
wa Baraza Kuu la 69, Bw. Sam Kutessa .
Mwakilishi
wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
akiwa na Afisa Mkuu Siongelael Shilla wakati wa upitishaji wa Azimio
namba A/69/L.85 kuhusu Ajenda 2030 ambapo baada ya kupitishwa kwa
kauli moja azimio hilo wazungumzaji wanaowakilisha makundi ya kikanda
walipata fursa ya kuelezea misimamo yao juu ya baadhi ya mambo ambayo
walikuwa wakitofautiana kimtizamo na kimsimamo.
Na Mwandishi Maalum, New York
AFRIKA, imesisitiza na
kubainisha kwamba itatekeleza malengo mapya ya maendeleo endelevu
kwa kuzingatia maslahi, vipaumbele, sera, mila na tamaduni ambazo
nchi za Afrika zimejiwekea.
Aidha Afrika
inasema kuwa, utekelezaji wa malengo hayo pia utazingatia sheria
za kimataifa na ambazo nchi za Afrika zimeridhia na si vinginevyo.
Hayo
yameelezwa na Balozi Fode Seek, Mwakilishi wa Kudumu wa Senegal
katika Umoja wa Mataifa ambaye ni Mwenyekiti wa nchi za Afrika kwa
mwezi Septemba.
Alikuwa akizungumza kwa niaba
ya nchi za Afrika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
lilipokutana siku ya jumanne, kupitisha Azimio namba A/69/L.85 ambalo
linawasilisha ajenda ya Maendeleo Endelevu (ajenda 2030)
itakayotekelezwa kwa miaka 15 ijayo.
Ajenda 2030 inachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayofikia ukingoni mwishoni mwa mwaka huu.
Kupitishwa
kwa azimio hilo la ajenda 2030, inayojumuisgha malengo 17 na ambalo
sasa litawasilishwa baadaye mwezi huu wa Septemba kwa Viongozi Wakuu
wa Nchi na Serikali tayari kwa kuridhiwa na kuanza utekelezaji wake
mwakani, kunakamilisha mchakato uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili ya
majadiliano yaliyozaa malengo mapya na ajenda mpya.
“Afrika itashirikiana
na wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa malengo
haya yanayolenga katika kuondoa umaskini, kuboresha huduma za
jamii, upatikanaji wa fursa za maendeleo na ajira na bila ya kumwacha
yoyote nyuma. Lakini tutatekeleza kwa kuzingatia mipango yetu,
vipaumbele vyetu, sera zetu na kwa maslahi ambayo ambayo kila nchi
itaona inafaa kutoka na mazingira na uwezo wa nchi yenyewe” akasema
Balozi. Seek
Baadhi
ya mambo ambayo Afrika inasema kimsingi haikubaliani katika ujumla
wake na ambayo kwayo utekelezaji wake utazingatia utashi wa kila
nchi, kuzingatia Imani za kidini, mila na tamaduni na sheria za
nchi husika ni pamoja na tafsri sahihi ya neno familia ambalo Afrika
na baadhi ya nchi nyingine inasema familia ni Baba, Mama na watoto
na si tafsili ile inayopigiwa chapuo na baadhi ya nchi za magharibi.
Jambo jingine
ambalo Afrika na Nchi nyingine imetoa msimamo , linahusu
tafsiri ya jinsia ambayo kwa Afrika inaamini kwamba jinsia ni ya kike
na kiume.
Utolewaji na
upatikanaji wa huduma za afya, elimu na mafunzo yanayoambatana na
eneo hilo na hususani uzazi wa mpango, ni eneo jingine ambalo Afrika
na mataifa mengine yanayoendelea yanasisitizia kuwa utekelezaji wake
usiwe wa shurutisho na ufanyike kwa kuzingatia mila na desturi za nchi
husika.
Mbali
ya msemaji huyo kwa niaba ya nchi za Afrika kuanisha baadhi ya maeneo
ambayo Afrika itayatekeleza pasipo
kushurutishwa. Wazungumzaji zaidi ya 30 wakiwakilisha makundi
ya kikanda na baadhi wakizungumza kwa niaba ya nchi zao walichangia
maoni yao kuhusu ajenda 2030.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Afrika ya Kusini Balozi Kingsley Mamabolo ambaye
ni Mwenyekiti wa Kundi la G77& China. Akizungumza kwa niaba ya
kundi hilo anasema.
Haikuwa kazi nyepesi kufikia makubaliano yaliyopelekea kupitishwa kwa kauli moja Malengo na Ajenda 2030
“ Ajenda
hii ambayo tumeipitisha kwa kauli moja, hatuwezi kusema kwamba haina
mapungufu. lakini tumefika hapa tulipo baada ya majadilliano marefu na
magumu na kukubaliana kuto kukubaliana”.
Na akaongeza Ajenda
2030 ina mambo mengi yakiwamo malengo 17 na viashiria 169. Lakini
jambo moja la msingi na muhimu ni kwamba, utekelezaji
wake utategemea kila nchi inavyopanga vipaumbele vyake na sera zake”
akasema Balozi Mamabolo.
Awali
akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema. Agenda 2030 ni
makubaliano ambayo kila nchi inapashwa kujivunia na kwamba utekelezaji
wake utahitaji ushirikiano wa karibu baina ya wadau mbalimbali.
Akasema Agenda 2030
itapitishwa na Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa
mbalimbali duniani akiwamo Baba Mtakatifu Francis.
No comments:
Post a Comment