RPC
wa Mkoa wa Dodoma SACP. David A. Misime akiongea na waandishi wa Habari
leo akitoa tahadhari juu ya matapeli wanaowadanganya na kuwatapeli
wastaafu. LAPF kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
imefanikiwa kumkamata mtu mmoja na kumfikisha Mahakamani baada ya
kujifanya ni mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA
YA AFYA na kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu
kutoka katika mikoa mbalimbali.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa ufafanuzi katika mkutano huo na waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 02.09.2015
MFUKO wa Pensheni wa LAPF unapenda
kutoa kutoa tahadhari hasa kwa Wastaafu au wanaotarajia kustaafu,
Idara, Wizara zote zinazoshughulika na wastaafu, Wakurugenzi wa Manispaa
na Halmashauri kujihadhari na watu wanaowapigia simu na kujitambulisha
kuwa wao ni watumishi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii na Idara zingine
za Serikali na kwamba wanashughulika na mafao ya wastaafu.
LAPF
inatoa tahadhari hiyo kwa sababu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa jina la DAVID MAGESA
MAKALI @ PETER MABULA na kumfikisha Mahakamani baada ya kujifanya ni
mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA na
kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika
mikoa mbalimbali.
Wanachofanya
watu hao wanapiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au
Wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani
pamoja na namba zao za simu. Inaonyeha kwa njia hiyo wameweza kupata
orodha ya wastaafu takriban kutoka katika Mikoa 15 hususan kutoka Idara
ya afya.
Wakishapata
orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu humpigia mstaafu na
kujitambulisha anatokea Wizarani na anashughulikia wastaafu ambao
inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonyesha naye amepunjwa
kiasi cha milioni fulani.
Ili
aweze kumsaidia kurekebisha kumbukumbu na kumwezesha kupata fedha hizo
amtumie kiasi fulani cha fedha. Mstaafu huyo akishamtumia hapatikani
tena kwenye hiyo namba aliyotumia na mstaafu huyo anakuwa ameishaibiwa
fedha zake.
LAPF
inatoa tahadhari kwa wastaafu wasikubaliane na watu wa aina hiyo na
idara mbalimbali zichukue tahadhari kubwa na kila mara wahakikishe
kinachohitajika kinatoka katika idara husika na kwa mtu sahihi.
Mfuko
wa Pensheni wa LAPF unaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama na
wastaafu wake na katika kuhakikisha kuwa tunamlipa jana mstaafu wa
kesho. LAPF inawakumbusha wanachama wake wanaokaribia kustaafu
kuwasilisha mapema maombi ya mafao ya kusataafu (miezi sita kabla ya
kustaafu) ili tuweze kuandaa mafao mapema.
LAPF
ni Mfuko wa Pensheni ambao pamoja na majukumu mengine, jukumu lake kuu
ni kutoa mafao ya Pensheni kwa wanachama wake. Mafao yanayotolewa na
LAPF ni pamoja na;
· Pensheni ya Uzeeni.
· Pensheni ya Ulemavu.
· Pensheni ya Urithi.
· Fao la Uzazi.
· Mikopo ya kujikimu.
· Mikopo ya elimu .
· Mikopo ya nyumba.
· Mikopo kwa wanachama wa kupitia Saccos.
· Mikopo kwa Wastaafu.na
· Msaada wa mazishi.
Kwa
sasa Mfuko wa pensheni wa LAPF unaandikisha wanachama kutoka sekta zote
kama vile Waalimu, Watumishi wa Afya, Wajasiliamali nk.
Imetolea na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
No comments:
Post a Comment