Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Donani Mmbando akizungumza na waandishi
wa habari hawapo pichani juu ya Mfumo
unahifadhi na kutoa taarifa za zituo vya Afya kituo tangu kinapojengwa, atakikifunguliwa
na hata kinapofungwa, leo Jjijini Dar es salaam.
Wanahabari wa kimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Donani Mmbando leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Donani Mmbando akifafanua jambo leo Jjijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Wizara ya Afya na
Usitawi wa Jamii Hermes Rulagirwa towa ufafanuzi kwa waandi wa habari juu ya mfumo
wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma za afya vya serikali na binafsi leo jijini Dar es salaam.
SehemU ya wananchi walio hudhulia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Donani Mmbando akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi mbalimbail leo Jjijini Dar es salaam .
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetengeneza
mfumo wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma za afya vya serikali na binafsi “Health
Facility Registry (HFR) System”.
Mfumo unahifadhi na
kutoa taarifa za kituo tangu kinapojengwa, ili kimejengwa, kufunguliwa na hata
kinapofungwa. Zaidi tunapata taarifa ifutayo;-
Idadi ya vituo Tanzania
bara, taarifa za kijiografia (yaani“Geographic coordinates), mahali kituo kilipo,
kwa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Mtaa/kijiji, umiliki, hali ya utendaji kazi yaani
“operation status” na huduma inayotolewa na kituo.
Kutokana na kukamilika
kwa mfumo huu, naagiza Taasisi zetu kama NHIF, MSD, NACP, TFDA pamoja na wadau
wengine waanze kutumia mfumo huu.
Mfumo huu umetengnezwa
kwa ufadhiri wa mfuko wa ukimwi kifua kikuu
(Global fund) CDC, RTI Intenational. Pia natambua Ushiriki wa wadau
wetu, University Computing Centre, Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Aidha mfumo huu
umetengenezwa kwa kushirikisha idala zote za Wizara na Taasisi zake. Hivyo ni
mfumo shirikiskishi na una ownership.
Nawapongeza pia wajumbe
wa kamati ya Afya za Mikoa na Wilaya, kwa kufanikisha, ukamilikaji wa mfumo
huu.
Naagiza kwenu nyinyi
waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kuhakikisha mnasimamia kwa kuingiza taarifa
kwa wakati.
Baada ya kusema hayo,
natangaza kuwa mfumo huu wa mfumo wa utunzaji wa taarifa za vituo vya afya
tanzania bara, umezinduliwa rasmi.
No comments:
Post a Comment