WAKULIMA ZAIDI YA 12,000 KUNUFAIKA NA MBEGU BORA ZA MAHINDI NA ALIZETI MKOANI - LEKULE

Breaking

10 Sept 2015

WAKULIMA ZAIDI YA 12,000 KUNUFAIKA NA MBEGU BORA ZA MAHINDI NA ALIZETI MKOANI

Baadhi ya wakuliwa wa mkoani Shinyanga, wakiwa na maofisa wa Agrics wakati wa mafunzo na uingiaji mkataba wa makubaliano yliofanyika Kijiji cha Ishololo, Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Warsha hiyo iliongozwa na Lazaro Japhet (aliyesimama wa tatu kushoto mstari wa mbele. Zaidi ya wakulima 12,000 wanataraji kufaidika na mbegu za mahindi na alizeti kutoka Kampuni ya Agrics.
Mahindi yaliyooteshwa kisayansi na kampuni ya Agrics kwa lengo la kuthibitisha ubora wa mbegu zinazotolewa kwa wakulima wa kanda ya ziwa. Zaidi ya wakulima 12000 watanufaika na mbegu izo msimu huu. Matokeo ya vipimo yalisadifu ubora wa kampuni ya Agrics kwa kutoa asilimia 100% ya ubora.

Kufuatia msimu mpya wa kilimo unaotarajia kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics inatarajia kuwanufaisha wakulima 12,000 wa Shinyanga vijijini, Maswa na Meatu kwa kuwapatia mbegu bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea ili kuhakikisha kilimo biashara kinainuliwa na kuleta tija kwa mkulima. Mbegu hizo zitatolewa hivi karibuni ili kuhakikisha mkulima anakuwa na maandalizi ya uhakika msimu huu. Kampuni ya Agrics hutoa mbegu kwa mkopo nafuu unaolenga kumnufaisha mkulima kwa mazao mengi zaidi.

Pia Agrics ikishirikiana na viongozi wa serikali huwanufaisha wakulima kwa kuwapatia mafunzo katika ngazi tofauti za ukuaji wa mazao ili kuhakikisha mavuno yanasadifu malengo ya wakulima hao.

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya Agrics, Meneja Miradi Bw. Charles Laswai alithibitisha ubora wa mradi huo wakati akikabidhi mikataba ya uchaguzi wa mbegu kwa wakulima. ‘’ Ni miaka mitano sasa tangu Agrics ianze kutoa mbegu bora kwa mkopo kwa wakulima wetu wa kanda ya ziwa.

Kwa sasa wakulima wameelewa zaidi umuhimu wa kilimo biashara. Mkulima anavuna zaidi ya asilimia arobaini kulinganisha na kabla ya kujiunga na mradi huu wa kukopeshwa mbegu na mbolea kwa ajili ya kilimo bora. Na kwa mwaka huu tunategemea mavuno mazuri zaidi kwani hali ya hewa itakuwa nzuri kutokana na vyanzo vya taarifa ya hali ya hewa nchini’’.

Wakulima wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa mikopo kwa ajili ya kilimo na ukosefu wa elimu juu ya kilimo bora chenye tija. Agrics ikiwa kama chachu ya mabadiliko kwa mkulima wa kanda ya ziwa, imekuwa ikiwakopesha mbegu na mbolea zilizothibitishwa kwa ubora, mkulima hutoa asilimia kumi wakati wa kuomba aina ya mbegu aitakayo na badae hutoa asilimia 15 wakati wa kukabidhiwa mbegu husika.

Mkulima hupewa nafasi ya kuwa huru na kusimamia kilimo chake huku akiendelea kupata mafunzo na ushauri kutoka kwa afisa miradi wa Agrics ili kuhakikisha malengo ya mkulima yanatimia na anazalisha kwa kiasi kikubwa. Mkulima humalizia asilimia 75% ya deni lake kwa awamu tatu zinazompa muda wa kutosha baada ya kuwa amevuna.

“Ni kampuni ya Agrics iliyoyabadilisha maisha yangu kufikia mafanikio haya niliyonayo. Kiujumla wamebadilisha maisha ya wakulima wa hapa kijijini na kutufanya tuuage umasikini. Nilikuwa nikivuna gunia nne katika hekari moja lakini kwa sasa navuna zaidi ya gunia kumi kulingana na muitikio wa mvua. Tangu kujiunga na Agrics nimewapeleka watoto watatu sekondari na ninamiliki pikipiki kutokana na mavuno yangu. Sijawahi kuishiwa chakula kwani huwa ninaweka SIMIYU NA SHINYANGA.

akiba ya kutosha kwa ajili ya familia yangu’’. Alieleza Bw. Steven Kanogu mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga vijijini wakati akipokea mkabataba wa mkopo wa mbegu na mbolea kwa ajili ya kilimo cha msimu huu.

Agrics Ltd ni kampuni ya kibiashara inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na shirika la ICS. Agrics inawapa wakulima wadogo wa kanda ya ziwa nchini Tanzania na Kenya fursa ya kujipatia mbegu bora na za kisasa kwa mkopo nafuu unaolipwa kwa awamu zinazompa mkulima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Pia Agrics inahakikisha akiba ya chakula kwa mkulima ni lazima kwa ajili ya kupunguza njaa kwa wakulima. Kwa mawasiliano Zaidi tembelea tovuti yetu www.agrics.org.

No comments: