Mkurugenzi
wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura akiongea
kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza tukio hilo, ameeleza
Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la madhimisho ambayo
yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa habari waliowezeshwa na
misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani zimechangia kuleta
uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha kiwango cha
mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala bora na haki za
binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi waliowezeshwa na
TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Tukio
hilo litawaleta pamoja waandishi wa habari na wanataaluma wengine ambao
wamewezeshwa na misaada ya TMF, wafadhili, wadau wa sekta ya habari
pamoja na taasisi za kiraia na serikali. Akiongea kwenye mkutano na
waandishi wa habari kutangaza tukio hilo, Mkurugenzi wa TMF, Ernest
Sungura alisema: “Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la
madhimisho ambayo yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa
habari waliowezeshwa na misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani
zimechangia kuleta uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha
kiwango cha mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala
bora na haki za binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi
waliowezeshwa na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Vile
vile kutakuwa na mjadala utakaohusisha wataalamu wa habari na
wanaharakati kutoka asasi za kiraia katika kujadili changamoto
mbalimbali kama vile kuwajengea uwezo wanahabari na pia kuweka mazingira
endelevu na uhuru wa habari.
Sasa
ni miaka nane tangu TMF ilipoanzishwa na tumetoka mbali. Maadhimisho
haya yatatupatia fursa ya kutafakari kwa pamoja tulipotoka, mambo
tuliyoyafanya na pia tutapeana changamoto kufikiri zaidi jinsi ambavyo
sekta ya habari nchini Tanzania inaweza kubadilishwa ili kukuza
uwajibikaji.” Tangu ilipoanzishwa mwaka 2008, TMF imetoa misaada na
kuwawezesha waandishi wa habari zaidi ya 570 na zaidi ya taasisi za
habari 120.
Katika kipindi hiki, TMF imehusika na kuunga mkono jitihada za wadau
wengine wa habari na asasi za kiraia katika kukuza uhuru wa habari.
Mtandao wa TMF umevuka jiji la Dar es salaam na kufikia pembe zote za
nchi na unawagusa viongozi waandamizi wa vyombo vya habari pamoja na
waandishi waliopo maeneo yote ya nchi. Uchambuzi wa TMF kuhusu taarifa
mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari unaonyesha kwamba habari
ambazo zimefadhiliwa na TMF zimegusa masuala ya vijijini kwa kiwango
kikubwa. Asilimia 82 ya misaada ya TMF uelekezwa ukilinganisha na
asilimia 25 iliyoelekezwa kwenye habari za mijini.
Vilevile
uchambuzi umeonyesha kwamba taarifa zilizofadhiliwa na TMF huwa na
ubora wa hali ya juu ukilinganisha na taarifa za kawaida zinazoandikwa
au kutangazwa na vyombo vya habari nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
TMF, maadhimisho hayo pia yatatumika kuzindua Tanzania Media Foundation,
taasisi mpya ambayo itachukua nafasi ya Tanzania Media Fund ambao ni
mradi ulioanzishwa na wafadhili.
“TMF
mpya itakuwa ni mpango ulioanzishwa na Watanzania na kufanya kazi katika
misingi ile ile kama mradi wa TMF lakini itaelekeza nguvu zaidi katika
kuhakikisha yanakuwepo mazingira endelevu kwa ajili ya ukuaji wa TMF
pamoja na wanahabari wanaosaidiwa na TMF.
Tutaanzisha
upya mpango wa kuwezesha upatikanaji wa habari ambazo zina maslahi
makubwa ya taifa. Tutafanya kazi na wazalishaji vipindi ili kuongeza
habari za ndani ili kuvisaidia vituo vya televisheni kutimiza wajibu wa
kisheria kama ilivyoagizwa na TCRA ya kuwa na vipindi asilimia 60
vinavyohusu masuala ya ndani.
Tunataka
kuhakikisha vituo vya habari vinatoa habari za kukidhi mahitaji
mbalimbali.” “Tanzania Media Foundation itaanza kazi kwa kukutana na
wadau mbalimbali wa habari nchi nzima na itafanya nao kazi ili kutambua
habari ambazo zitaleta mabadiliko chanya katika jamii.”
No comments:
Post a Comment