Wateja
wa kampuni ya Tigo sasa wanaweza kutuma na kupokea fedha kupitia simu
zao za mkononi kirahisi na kwa haraka kutokana na maboresho makubwa
ambayo kampuni hiyo imefaniyia huduma yake ya Tigo Pesa.
Hii
ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Tigo jijini Dar es Salaam
kwa vyombo vya habari ikisema kwamba maboresho hayo pia yamerahisiha
ulipiaji wa ankara za huduma mbalimbali ikilinganishwa na ilivyokuwa
kabla.
“Tunayofuraha
kuwatangazia wateja wetu kwamba baada ya zoezi la maboresho kukamilika
kwa ufanisi sasa huduma za Tigo Pesa zimerejea,” ilisema taarifa hiyo.
Huduma za Tigo Pesa zilisitishwa usiku Jumamosi, Septemba 12 hadi
Jumapili mchana, Septemba 13 ili kufanya majaribio ya maboresho ya
mtandao.
Tigo Pesa ni huduma maarufu ya kifedha ikiwa na wateja zaidi ya milioni nne nchini kote.
Huduma
zinazotolewa na Tigo Pesa ni kutuma na kupokea fedha miongoni mwa
wateja wa Tigo na kwa wateja wa mitandao mingine ya simu, kuhamisha
fedha kutoka kwenye akaunti ya simu kwenda benki na kutoka kwenye
akaunti ya benki kwenda simu ya mkononi, kulipia huduma mbalimbali.
Mwaka
jana Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kuanzisha huduma ya kutuma
na kupokea ya kimatifa kwenda nchini Rwanda baina ya watumiaji wa Tigo
Pesa nchini na Tigo Cash nchini Rwanda. Tigo pia ilikuwa ya kwanza mwaka
2014 duniani kuanza kulipa faida kwa watumiaji wa Tigo Pesa kutokana na
kiasi cha amana kilichoko katika akaunti ya mteja. Malipo haya
hufanyika kila baada ya miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment