Msanii
wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Nature jana ameongea na Waandishi wa
Habari juu ya Ufanyaji kazi wake katika kipindi hiki cha kampeni Ambapo
aliongozana na Mgombea Ubunge jimbo la Mbagala ambaye ni rafiki mkubwa
na jirani wa msanii huyo Ndg Issa Mangungu.
Juma
nature kwa sasa amerudi kufanya kampeni na chama cha mapinduzi CCM na
ameamua kuelezea nia ya kurudi CCM baada ya mashabiki kumuona katika
Majukwaa mengine ya vyama vya kisiasa.
Nature
amesema kuwa mziki ambao anaufanya ni Biashara lakini pia anafanya kwa
ajili ya Jamii yake ambayo inamzuuka na pia anaangalia sehem ambayo
anakubalika ivyo akiitwa sehem yeyote kufanya kazi anaenda anafanya kazi
maana mziki ndio ajira yake.
No comments:
Post a Comment