Alexis Tsipras akishangilia ushindi Ugiriki
Chama cha
mrengo wa kushoto nchini Ugiriki cha Alexis Tsipras kimerejea tena
madarakani nchini humo baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi.
Kwa kura
nyingi zilizopigwa, hazikuweza kutoa viti vya kutosha bungeni kwa chama
hicho kuunda Serikali huku Waziri mkuu Tsipras akiwa tayari amekubali
kuungana na mrengo wa kulia kuunda serikali.
Tsipras
amesema kuwa Ugiriki ilikuwa na kipindi kigumu lakini waliweza kupigana
ndani ya Ugiriki na hadi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya na kwamba
wataendelea na mapambano kuikwamua Ugiriki.
Kulikuwa na furaha miongoni mwa wafuasi wa chama hicho katika mji wa Athens.
Kiongozi
wa chama cha New Conservative Vangelis Meimarakis amekubaliana na
matokeo hayo,na kutoa tamko rasmi la kuunga mkono ushindi huo.
Akizungumza nje ya makao ya chama chake amesisitiza kuundwa serikali madhubuti.