Burkina Faso:"rasimu ya mkataba wa kisiasa ya kumaliza mgogoro” - LEKULE

Breaking

21 Sept 2015

Burkina Faso:"rasimu ya mkataba wa kisiasa ya kumaliza mgogoro”



Nje kidogo ya hoteli Laico ambapo mazungumzo yameendelea Jumapili hii, Septemba 20, 2015.
Nje kidogo ya hoteli Laico ambapo mazungumzo yameendelea Jumapili hii, Septemba 20, 2015.
Na RFI
Wasuluhishi wa ECOWAS wamependekeza Jumapili hii jioni mjini Ouagadougou “mkataba wa kisiasa wa kumaliza mgogoro”nchini burkina Faso, wakiazimia Michel Kafando aliyepinduliwa madarakani Alhamisi wiki iliyopita kuendelea na uongozi wa nchi na kutoa msamaha kwa wanajeshi waliohusika na mapinduzi.
Rais Macky Sall hatimaye amekuja jioni kuwasilisha, hapana makubaliano rasmi, lakini "mambo kadhaa ya maelewano" . Rasimu ya mkataba ambayo itawasilishwa Jumanne asubuhi katika mkutano wa dharura wa ECOWAS.
Je, rasimu mkataba inaazimia nini?
Kwanza, kurejeshwa kwa taasisi za uongozi wa mpito, ambazo zinaanzia kwa rais Kafando. Rasimu inaangazia hasa "kuachilia huru bila masharti watu wote wanaozuiliwa kufuatia matukio hayo."
Pointi kuu ya pili: kuendelea na mchakato wa uchaguzi, lakini kwa uchaguzi wa rais na wabunge utakaofanyika kabla ya Novemba 22. Katika kipindi hiki, serikali na CNT (bunge la mpito) watakua hawana majukumu katika maandalizi ya uchaguzi na utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa.
Pointi ya tatu: uwezekano kwa wagombea wanaounga mkono Compaoré kuwania katika uchaguzi, wakati ambapo hapo awali walikuwa wametengwa.
Nakala itakayowasilishwa kwa marais kutoka Ukanda huo pia inaeleza "kukubaliwa msamaha na sheria ya kutoa msamaha juu ya matukio yaliyotokana na mapinduzi ya kijeshi." Sheria hii inapaswa kupitishwa kabla ya Septemba 30.
Na kisha kutakua na hatima ya wanajeshi wa kikosi cha usalama wa Rais (RSP), ambacho kilihusika katika mapinduzi ya serikali Alhamisi iliyopita. Katika rasimu iliyotolewa Jumapili hii, suala hili litajadiliwa baadaye. "Litajadiliwa na Rais atakayeatakaye chaguliwa katika uchaguzi ujao."
Rasimu kutopitishwa kwa kauli moja
Siku tatu za majadiliano makali si hazitapelekea kuafikia makubaliano lakini tu mapendekezo ya kumaliza mgogoro. Marais kutokanchi wanachama wa ECOWAS watajadili mapendekezo hayo katika mkutano wa dharura Jumanne ijayo. Mapendekezo ambayo yako mbali kupitishwa kwa kauli moja.
Baadhi wanasema mapendekezo hayo yanafuta mapinduzi ya kijeshi na yanapendekeza kutoa msamaha kwa wanajeshi waliohusika na mapinduzi hayo na kuwashirikisha wagombea wanaounga mkono Compaoré katika uchaguzi ujao, ambapo serikali ya mpito ilikua imewatenga. Madai makubwa ya jenerali Gilbert Diendéré.
Wengine wanasema kwamba mapendekezo hayo yanapelekea kuwepo kwa uwiano na kumrejesha Michel Kafando katika uongozi wa mpito kabla ya Septemba 30, na kuwaachilia huru wat wate wanaozuiliwa jela tangu mapinduzi ya Septemba 17.
Ushindi mwingine kwa wanajeshi waliofanya mapinduzi hayo, mageuzi yoyote ya jeshi yameahirishwa hadi baada ya uchaguzi, wakati ambapo mashirika ya kiraia na Spika wa Bunge la Mpito wamekua wakidai kuvunjwa kwa kikosi cha wanajeshi wa ulinzi wa Rais Usalama cha jenerali Diendéré.