Meneja wa
NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino (kulia) akikabidhi madawati kwa
Mkuu wa Wilaya ya Geita - Manzie Mangochie (kushoto) kwa niaba ya Shule
za Msingi Nyamkumbu na Ukombozi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya
shilingi milioni 10 kutoka Benki ya NMB katika hafla fupi iliyofanyika
mjini Geita jana ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
Wanafunzi
wa Shule za Msingi Nyankumbu wakiwa na nyuso za furaha baada ya
kukabidhiwa msaada wa madawati 50 na Benki ya NMB jana wilayani
Geita.NMB ilisaidia madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni 10
katika shule mbili za msingi za Nyamkumbu na Ukombozi ambapo kila shule
ilipata madawati 50
BENKI ya
NMB jana ilikabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi
milioni 10 kwa Shule za Msingi Nyankumbu na Ukombozi zilizopo mkoani
Geita ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
Msaada
huo umekabidhiwa na meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino
ambapo mkuu wa wilaya ya geita alipokea madawati hayo kwa niaba ya shule
hizo mbili za msingi.
“Madawati
haya tunayoyakabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya
jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii
inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema
Augustino.
No comments:
Post a Comment