“HATUSAMBAZI MAJI YENYE UCHAFU BUGURUNI”- DAWASCO - LEKULE

Breaking

9 Sept 2015

“HATUSAMBAZI MAJI YENYE UCHAFU BUGURUNI”- DAWASCO


SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wananchi kuepuka taarifa za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya usambazaji maji machafu kwenye line za mabomba ya wateja wa Dawasco.
Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro alisema taarifa hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili kuchafua taswira ya shirika hilo na pia kuihusisha Dawasco moja kwa moja na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.
“Tunawatahadharisha wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo vyote kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji yenye kuleta madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu kufanya hivyo ” alisema Lyaro.
‘Ukweli wa maeneo yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na Buguruni ni kuwa kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini kama ni ya watu binafsi au za manispaa.
Wao walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja walio na line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea mabomba ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu yaliyokatwa kutoka kwenye mifereji” aliongezea lyaro.
Alisema kuwa Baada ya kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni kuchukua sampuli za Maji hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji hayo yasiendelee kutoka. Na baada ya upimaji sampuli ile na kukuta sio salama tulitenga line(isolate) ya majisafi ya sharif shamba hadi hapo tatizo litakapotatuliwa na mamlaka husika.
Tuhuma za Dawasco kusambaza Maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku zikihusishwa zaidi na athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kushika kasi jijini dar.

No comments: