Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Katibu Mwenezi Wahamia CHADEMA...........Diwani wa CCM Mwanza na Wanachama 100 Wahamia CUF - LEKULE

Breaking

9 Aug 2015

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Katibu Mwenezi Wahamia CHADEMA...........Diwani wa CCM Mwanza na Wanachama 100 Wahamia CUF


Hali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na wanachama zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).
 
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa wimbi la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 
Diwani na wanachama hao kutoka matawi mbalimbali ya CCM, walieleza chanzo na sababu za kutimkia CUF, kuwa chama hicho kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na undugu kitendo kinachosababisha kukosekana kwa demokrasia ya kweli.

Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa kushika madaraka na kusababisha watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.
 
Wanachama hao wakiongozwa na diwani huyo, wamepokelewa  na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Chakechake, Nyamagana.
 
Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na kukosekana kwa demokrasia.
 

“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka waachane na wizi wao."  Amesema  Fashion.

Arusha  Hali  ni  Mbaya  Zaidi
Habari  kutoka  jijini  Arusha  zinaarifu  kuwa  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Mh Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha,Mh. Isack  Joseph  wamejiuzulu nafasi zao zote leo na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Wakiongea  na  waandishi  wa  habari  leo, viongozi  hao  wamemtaka  Katibu  Mkuu  wa  CCM, Mh Kinana  kuacha  mara  moja siasa  za  matusi za  kuwaita  Makapi  wanachama  ambao  wamekuwa  wakijiunga  na  vyama  vya  upinzani.


Ikumbukwe  kuwa,zaidi ya wanachama mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli juzi  walizichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA .


No comments: