Uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2015 utakuwa wa aina yake kufuatia matukio makubwa matatu makubwa kukoleza safari ya kumtafuta rais ajaye kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Matukio
hayo ni pamoja na (a) Vyama vya Upinzani kuungana (b) Waziri mkuu wa
zamani CCM kuhamia Upinzani-Edward Lowassa (c) Vijana wengi
kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Matukio
hayo matatu yamebadilisha siasa za Tanzania kwa mwaka huu huku
kujitokeza kwa vijana kujiandikisha kuna ashiria mwamko mkubwa walio nao
hivisasa katika kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri haki yao ya kikatiba
ya kupiga kura tarehe 25 mwezi oktoba mwaka 2015.
Watalaamu
mbalimbali wa masuala ya kisiasa nchini na nje ya nchi wamebainisha
kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti na chaguzi za miaka ya
nyuma hivyo basi mabadiliko hayo yanaonesha kukua kwa demokrasia
ambayo inasema kwamba Wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na
wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma kwa
kufuata misingi ya katiba ya nchi.
Utafiti
mdogo uliofanywa na Mpekuzi umebaini kuwa wagombea wawili wamekuwa
katika mchuano mkali miongoni mwa wananchi mbalimbali ndani na nje ya
nchi.
Wagombea hao ni yule wa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Edward Lowassa kupitia umoja wa katiba ya wanchi yaani UKAWA.
Wagombea hao ni yule wa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Edward Lowassa kupitia umoja wa katiba ya wanchi yaani UKAWA.
Katika
mitaa mbalimbali hivisasa Vijana wana msemo wao unaosema “Habari ya
mjini”, hivyo habari ya mjini hivisasa ni Lowassa na Magufuli kugombea
urais.
Katika
moja ya mtaa jijini Dar es salaam mwandishi wetu ameshuhudia mabishano
makali ya nani zaidi kati ya Lowassa na Magufuli huku kila upande
ukitamba mgombea wake ni zaidi ya mwingine.
Kwa
kiasi kikubwa mabishano hayo yamekuwa hasa upande wa utendaji
serikalini pamoja na kukubalika kwao kwa ujumla katika jamii pamoja na
sera za kila chama kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania kwa kipindi
cha miaka mitano ijayo.
Inadaiwa
kuwa kuna baadhi ya maeneo ukimsema vibaya mmoja wa hao wagombea
wawili ambao ni Lowassa na Magufuli unaweza ukaambulia kipigo.
No comments:
Post a Comment