Afisa Madini Mkazi- Kigoma, Adam Juma akifungua mafunzo hayo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao kwa wachimbaji madini wa Mkoani Kigoma (hawapo pichani). Kushoto kwake ni wataalamu kutoka Wizarani-Kitengo cha Leseni Idd Mganga akifuatiwa na Mhandisi Edward Mumba. Kulia kwake ni Viongozi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo Kigoma (KIGOREMA), Karoli Ndimaso na Augustino Ruronona.
Hatimaye mafunzo ya huduma ya leseni kwa njia ya mtandao kwa wachimbaji madini mkoani Kigoma yamemalizika. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wachimbaji madini zaidi ya mia moja.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Afisa Madini Mkazi- Kigoma, Adam Juma aliwataka wachimbaji madini mkoani humo kuhakikisha wanafika Ofisi za Madini-Kigoma kwa ajili ya kusajiliwa kwenye mfumo huo.
Alisema ni vyema wachimbaji hao wakafanya hivyo mapema ili waanze kutumia mfumo huo ili kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa tekonolojia duniani.
Baadhi ya wachimbaji madini Mkoani kigoma waliohudhuria mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kuelewa namna ambavyo mfumo huo unavyofanya kazi.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Mafunzo ya Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao (OMCTP) yaliyofanyikia Mkoani humo na kuhudhuriwa na wachimbaji madini zaidi ya mia moja kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo
No comments:
Post a Comment