Meneja
mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah,
akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano
yanayohudhuriwa na wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida.Wa
kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone na anayefuatia
ni,Dk.Willhelm Ngasamiaku,mhadhiri wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu
cha Dar-es-salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,akizungumza kwenye uzinduzi wa
mafunzo ya siku tano yanayohudhuiwa na wafanyabiashara wadogo 150
yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya
wananchi mjini hapa. Dk.Kone ameahidi kuwa serikali mkoani hapa
itaendelea kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara hao, ili shughuli
zao ziwe za tija zaidi.
Mhadhiri
wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam, Dk.Wilhelm
Ngasamiaku,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya
wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida yanayoendelea kwenye chuo
cha maendeleo ya wananchi mjini hapa.Wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa
Singida,Dk.Parseko Kone na wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya
Singida,Iddi Amanzi. Kushoto ni Meneja mradi wa kuwajengea uwezo
wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah.
Baadhi
ya wafanyabiashara wadogo mkoani Singida, wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa
Singida, Dk.Parseko Kone (hayupo pichani),wakati akizindua mafunzo ya
wafanyabiashara hao.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa pili kulia walioketi) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo ya wafanyabiashara
wadogo.Kulia aliyeketi ni mkuu wa wilaya ya Singida,Idd Amanzi.Wa tatu
kushoto waliosimama,ni Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara
wadogo,Florentina Sallah na aliyeketi kushoto, ni mhadhiri wa uchumi
chuo kikuu cha Dar-es-salaam,Dk.Wilhelm Ngasamiaku.
SERIKALI
mkoani Singida, imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia
shughuli za wajasiriamali mbalimbali, ili shughuli zao ziweze kuwa zenye
tija zaidi.
Ahadi
hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,wakatai
akizindua mafunzo ya wafanyabiashara wadogo 150 mkoani hapa
yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi (FDC) mjini hapa.
Alisema
serikali kwa upande wake imewajengea wajasiriamali mazingira rafiki na
mazuri ya kufanyia shughuli zao zikiwemo za kilimo cha mbogamboga na za
kuzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
“Miaka
michache iliyopita, serikali imeweza kugoresha na kujenga barabara za
kiwango cha lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa mia nne. Pia
imehakikisha mawasiliano mazuri ya simu za viganjani yanapatikana kwa
urahisi karibu sehemu zote za mkoa wetu wa Singida”, alifafanua Dk.Kone.
Akiongezea,
alisema wajasiriamali mkoni hapa,kwa sasa wanatumia barabara za lami
kufikisha mazao na bidhaa zao kwenye masoko ya uhakika kwa urahisi na
kwa muda mfupi mno.
“Wajasiriamali
vile vile wanatumia simu zao za viganjani kutafutia masoko nadani na
nje ya nchi.Kwa kutumia mawasiliano hayo wamekuwa wakiagiza bidhaa na
kuletewa mahali walipo bila wao kusumbuka kwa kuzifuatia”,alisema.
Aidha,
Dk.Kone alisema serikali mkoani hapa itajitahidi kuhakikisha
wajasiriamali wanapata mazingira salama na utulivu kwa ajili ya shughuli
zao na kuwasaidia kurasimisha biashara zao,ili klungeza tija na kipato
chao pia.
Katika
hatua nyingine,mkuu huyo wa mkoa, amewataka wajasiriamali hao wawe
mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawajapata bahati ya kupata mafunzo
hayo.
“Ni
imani yangu kuwa mtakwenda kuwafundisha wenzenu faida na umuhimu wa
kurasimisha biashara zao huku mkiwaeleza hasara za kufanya biashara
katika mazingira yasiyo rasmi”,alisema mkuu huyo wa mkoa.
Dk.Kone
ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa ESAURP (Eastern and Southern
African Universities Research Programe) kwa kugharamia mafunzo hayo na
kuuomba uendelee kuleta mafunzo zaidi ya aina mbalimbali.
Awali
meneja wa mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo pamoja na
kuwarasimisha, Florentina Sallah, alisema mradi huo unatekelezwa katika
mikoa 10 hapa nchini.
Alisema
madhumuni na malengo ya mradi huo,ni pamoja na kuwapatia mafunzo
wafanyabiashara wadogo yatakatowasaidia kuondokana na kufanya biashara
katika mfumo usio rasmi, na kuanza kutumi mfumorasmi utakaowasaidfia
kuwatambulisha na wadau mbalimbali wakiwemo wa taasisi za kifedha.
No comments:
Post a Comment