Pierre Nkurunziza ameapishwa kwa muhula wa tatu, lakini sherehe za kuapishwa zasusia na jumuiya ya kimataifa, Bujumbura, Agosti 20
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amemeapishwa Alhamisi wiki hii kwa kuliongoza taifa hilkwa muhula wa tatu unaoendelea kuzua utata.
Pierre Nkurunziza angeliapishwa Agosti 26, kwani ndio siku muhula wa pili ungelikua umetamatika. Lakini Pierre Nkurunziza na washirika wake wa karibu wamebaini kwamba wamefanya hivyo kutokana na mdororo wa usalama unaoendelea kushuhudiwa nchini mwao.
Watu wachache wamehudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa rais Pierre Nkurunziza. Wawakilishi kadhaa wa nchi za kigeni, ikiwa ni pamoja na mabalozi mbalimbali wamesema walipata taarifa ya kuapishwa kwa rais huyo katika dakika ya mwisho kwa njia ya simu. Hata waandishi wa habari wa kituo cha runinga vya serikali wamepewa taarifa hiyo mapema leo Alhamisi asubuhi. Ili kujitetea kuhusu haraka hiyo ya kuapishwa kwa rais, viongozi nchini Burundi wameelezea "sababu za kiusalama".
Tangu kifo cha jenerali Adolphe Nshimirimana, hali ya taharuki imeendelea kutanda katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura na uvumi umekua ukienezwa katika mji huo zikisalia siku chache kabla ya Agosti 26, tarehe ambayo angeliapishwa rasmi. Kila mtu amekua akijiuliza siku na jinsi gani rais huyo ataapishwa. Matokeo yake ni kwamba viongozi wamewashitukiza watu wote, ametathimini Alhamisi asubuhi wiki hii mwangalizi wa mgogoro wa Burundi.
Sherehe zasusiwa na jumuiya ya kimataifa
Hakuna marais au viongozi wa nchi za kigeni ambao walikuwepo katika sherehe za kuapishwa rais Pierre Nkurunziza. Nchi kadhaa zimewamtuma mabalozi wao, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, China na Urusi, ambao mabalozi wao walikuwa kwenye nafasi ya kwanza.
Nchi za Ulaya kwa upande wao, hivi karibuni mjini Brussels zilipitisha msimamo mmoja, kuwa zitawakilishwa katika sherehe za kuapishwa Pierre Nkurunziza na mabalozi wao pekee. Katika sherehe hizi za leo, nchi hizo zimewakilishwa na wanadiplomasia wa cheo cha chini. Hivyo hivyo kwa nchi ya Marekani, ambayo imewakilishwa na namba 2 wa ubalozi. Ikumbukwe kwamba Umoja wa Ulaya na Marekani waliutaja uchaguzi huo kwamba si wenye kuaminika. Hata hivyo, Umoja wa Afrika haukuwakilishwa katika sherehe hizo, kwani umefutilia mbali mwaliko wa viongozi wa Burundi.
Serikali ya Umoja
Katika hotuba yake ya kuapishwa, Pierre Nkurunziza amezungumzia uwezekano wa marekebisho ya Ibara ya 129 ya Katiba, ili kuunda serikali ya Muungano. Kutokana na matokeo uchaguzi wa wabunge, sheria ya sasa haimruhusu Pierre Nkurunziza kumteua mtu yeyote kutoka chama kingine kuliko chama chake. Ibara ya 129 pia inaeleza kwamba serikali inapaswa kuundwa kwa misingi ya kikabila, ikiwa ni pamoja na asilimia 60 ya Wahutu na asilimia 40 ya Watutsi, kulingana na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.
Upinzani nchini Burundi ambo ulitaja hivi karibuni kuwa uchaguzi wa rais huyo ni "kinyume cha sheria" umemuonya Nkurunziza atapoteza majukumu yake mara tu atakapo apishwa.
Wakati huo huo, rais Nkurunziza amemteua Gaston Sindimwo kutoka chama cha UPRONA mshirika wa karibu wa chama tawala cha CNDD-FDD, kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Wakati huo huo, rais Nkurunziza amemteua Gaston Sindimwo kutoka chama cha UPRONA mshirika wa karibu wa chama tawala cha CNDD-FDD, kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Chama hicho cha Uprona hakikufikisha asilimia tano katika uchaguzi wa wabunge, na kulingana na Katiba hakingilipaswa kushirikishwa katika serikali.
No comments:
Post a Comment