Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hakuna mtanzania aliyewahi kufa njaa kwani nchi haikuwahi kuwa na upungufu wa chakula na kusababisha hali ya kuleta athari za kifo kutokana na njaa kwa wananchi wake.
Dkt.
Kikwete aliyasema hayo jana mjini Lindi wakati akiwahutubia watanzania
katika maadhimisho ya kitaifa ya sikukuu ya wakulima nanenane
yaliyofanyika mkoani humo
Dkt.
Kikwete alisema kinachofanyika sasa ni kuhakikisha wakulima wanalima
mazao mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko zaidi ya ndani
na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya kilimo kwa kukuza uchumi na
kuwaondolea watanzania Umasikini.
Aliongeza
kuwa licha ya Uzalishaji kuongezeka lakini bado Serikali haijafika
inapopataka hivyo haina bundi kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea sekta
ya kilomo iwe yenye tija zaidi.
Katika
maadhimisho hayo Dkt. Kikwete alitumia nafasi yake kuwaaga wakulima
ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza muda wake madarakani, huku
akiwataka watanzania kutumia vyema haki yao ya kupiga kura na kumchagua
kiongozi wanaempenda
No comments:
Post a Comment