Meneja
wa Vifaa vya Huawei, Peter Zhang Nchini (kulia), akionesha aina ya
simu ya Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika
matumizi ya nyanja mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa simu hizo. Kushoto ni Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga.
Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa ya uzinduzi huo.(P.T)
KAMPUNI
ya Mawasiliano ya Tigo na ile ya kutengeneza simu za mkononi ya Huawei,
wameshirikiana kuzindua simu mpya mbili za kisasa kwa ajili ya watumiaji
wa simu za hali ya chini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa
Vifaa vya Huawei, Peter Zhang alizijata simu hizo ni Huawei Y 360 na Y
625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja
mbalimbali.
Alisema
simu hizo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo mwananchi yeyote atakuwa na
uwezo wa kununua kwa ajili ya kwenda na kasi ya teknolojia ya digitali.
Kwa
upande wa Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga alisema
wanaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania ili wote waweze kuwa
kwenye digitali na kwa kuzindua simu hizo itasaidia jamii kuingia kwenye
ulimwengu huo.
Alisema
wateja wanaotumia mtandao wao watakaponunua simu hizo watapata ofa
mbalimbali zitakazowasaidia kuendelea kupata huduma zikiwemo vifurushi
na kusikiliza muziki bure kwa miezi sita.
No comments:
Post a Comment