Dar es Salaam.
Wakati vyama vinne vinavyounda Ukawa, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine vya Sau na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Wakati vyama vinne vinavyounda Ukawa, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine vya Sau na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Pia Ukawa walimtangaza Juma Duni Haji kuwa mgombea mwenza wa Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea urais Zanzibar.
Katibu
Mkuu wa Sau, Ali Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga
mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki
alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo
wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo.
Mwenyekiti
wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini
mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono Ukawa.
“Uchaguzi
wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,000, lakini
pia tuna madiwani watatu na wanachama wameongezeka kwa hivyo ninaamini
mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa Ukawa,” alisema Mziray.
Mwenyekiti
wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema chama hicho
kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea mmoja kutoka CCM au Ukawa. “Nafasi
ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati ya vyama hivyo
wakati wa kampeni.”
No comments:
Post a Comment