Hali ni Mbaya: 7 Wafariki kwa Kipindupindu Dar, 230 Wamelazwa - LEKULE

Breaking

25 Aug 2015

Hali ni Mbaya: 7 Wafariki kwa Kipindupindu Dar, 230 Wamelazwa



Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini imesema watu 7 wamekufa kwa ugonjwa wa kipindupindu huku wagonjwa 230 wakilazwa katika kambi mbali mbali maalum katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid amesema kuwa kati ya wagonjwa hao 194 ni kutoka Dar es Salaam na 36 ni kutoka Mkoa wa Morogoro.

No comments: