Mgombea wa Urais wa Ukawa Edward Lowassa pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji leo wamewashitukiza wafanyabiashara katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.
Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda.
Kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara hao,Lowassa alikaribishwa chai na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.
Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba katika maisha yao ya kila siku.
Je, Unataka kufahamu kesho Lowassa atakuwa wapi? Endelea kufuatilia mtandao huu.
No comments:
Post a Comment