TMT 2015 YAZIDI KUNOGA - LEKULE

Breaking

21 Jul 2015

TMT 2015 YAZIDI KUNOGA


Majaji wa TMT, Rich, Monalisa na Roy Sarungi.

Kutoka kushoto ni Tomluck Stephan (Arusha) Vandeline August (Mbeya) Catherine Nicholaus (Dodoma) na Dennis Laswai

Wa kwanza (kutoka kushoto),Titus Maridhia (Dodoma) Isaya Ryoba (Dar) Nadhifa Haruna (Mwanza) pamoja na Sadam Nawanda (Mtwara)

Washiriki wengine wakiwa katika picha kutoka kushoto, Daniel Lufingo (Dodoma), Naomi Chuwa Mtwara, Aisha Katabazi (Mwanza) na Saidi Mbelemba wa Dar

Mshiriki wa TMT, Isaya Ryoba kutoka Kanda ya Pwani Dar es salaam aliyeaga mashindano hayo.

Waalimu wa washiriki wa TMT wa kwanza kulia, Dkt. Mona Mwakalinga, Issa Mbuya wa pamoja na Matron wa TMT House.

Washiriki wa TMT upande wa wanaume wakiwa katika picha ya pamoja.

Washiriki wa kike nao wakiwa katika picha ya pamoja.

SHINDANO la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 wiki hii limezidi kufikia patamu baada ya washiriki 15 kubaki kati ya 20 waliokuwa wameingia katika Jumba wakati wiki hii ikishuhudia surprise ya washiriki kupigiana kura wao kwa wao.

Washiki hao wa TMT kila wiki wanapata mafunzo ya sanaa kwa nadharia na vitendo kutoka kwa waalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni Dkt. Mona Mwakalinga na Issa Mbuya kisha hupewa ‘script’ ya kuigizia.

Majaji na walimu hupitia mapema ‘script’ hizo ili kuangalia ushiriki wa kila mmoja na kuona uwezo wake tofauti na siku zilizopita, kitu kinachoamua uwepo wa kila mshiriki.

Vilevile baada ya hapo mchujo kwa washiriki wawili hufanyika kwa ajili ya kuyaaga mashindano kwa aliye na kura chache na kuigiza chini ya kiwango.

Ili mshiriki unayempenda aendelee kubakia ndani ya Jumba la TMT 2015 na kumpa nafasi ya kushinda milioni 50, katika simu yako ya kiganjani, andika TMT, acha nafasi, namba ya mshiriki kisha tuma kwenda 0784367738.?

Majina na namba za washiriki katika mabano ni Nadhifa Haruna (01), Aisha Katabazi (02), Kalombo Amboni (04), Dennis Laswai (05),

Tomluck Stephan Shukuru (06), Catherine Nicholaus (07), Titus Maridhia (08), Daniel Lufingo (09), Vandeline August (11), Jackson Sakumi (12), Naomi Chuwa (13), Sadam Nawanda (14),
Mohamed Massanga (15), Saidi Bakari Mbelemba (16) na Rachel Michael (17).

No comments: