Balozi
wa Simba, Octa Mshiu akipokea Hati ya Ubalozi kutoka kwa Rais wa Simba
Evans Aveva. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani
Kajula.
Dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado
inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa
mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi
mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo
vya mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Simba Evans Aveva
alisema ‘’Katika kukuza wigo wake wa kuwashirikisha wapenzi wake katika
kuleta maendeleo ya klabu Simba Sports Club inazindua makakati wa
kuwashirikisha wapenzi wenye nia ya kuwa chachu ya maendeleo kwenye
klabu yao.
Simba ni klabu ya wanachama na wapenzi wa Simba, hili ndilo jambo
la msingi na kujivunia zaidi. Kwa msingi huu wigo wetu wa wapenzi
nimtaji muhimu katika kuetekeleza malengo mbalimbali ya klabu ya Simba.
Hivyo basi leo hii klabu ya Simba inazindua rasmi Mabalozi wa Simba,
hawa ni wapenzi wa Simba ambao wako tayari kushirikiana na klabu
katika kuleta maendeleo ya klabu yetu’’.
Aveva aliendelea kusema ‘’ Katika ahadi zetu wakati wa uchaguzi
tuliahidi kuwa tumenuia kwa dhati kuleta mapinduzi ya kimaendeleo ndani
ya Simba. Napenda kusema safari yakuendelea kuifanya Simba kuwa klabu
bora ndani na nje ya uwanja imepamba moto.
Kwa uhakika malengo mengii kiwemo la kujenga uwanja na kambi ya
mazoezi ya Simba sio ndoto. Kupitia mabalozi wa Simba na mikakati yetu
mingine ya utunishaji wa mapato tunaamini kwa dhati malengo yetu
tutayafikia.
Kihistoria Simba imekua ni timu yenye kutendana kufikiriki
maendeleo na kutumia nguvu za wapenzi na wanachama, tulianza kwa kuwawa
kwanza kujenga jengo la klabu, Mzee Dalali aliona mbali na kununua
uwanja Bunju, nasisi tutaanza ujenzi, hii ndio dhima ya uongozi ndani
ya Simba kupokezana vijiti vya maendeleo’’.
Kwa upande wake MkurugenziMtendajiwa EAG Group LTD ambao ni
washauri watekelezaji wa mikakati ya biashara na masoko wa Simba
ImaniKajula alisema ‘’Zoezi la kuteua mabalozi wa Simba ni endelevu na
litafika kila kona ya Tanzania. Hawa ni mashabiki ambao mawazo,
michango yao ya hali na mali, kutumia ushawishi wao kutaleta maendeleo
kwenye klabu yetu.
Hawa watakuwa mstari wa mbele kwenye Simba Week kuhamasisha
ufanyaji kazi za jamii na kushiriki kwa wapenzi na wapenda maendeleo
katika kusukuma maendeleo ya Simba.
Napenda kuwashukuru sana Mabalozi hawa kwa kutenga muda na kuwa
tayari kusaidia juhudi za kuiletea Simba maendeleo. Uongozi wangu
utakuwa bega kwa bega nanyi katika kazi hii adhimu.
No comments:
Post a Comment