TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA DODOMA, MARIAM MFAKI AFARIKI DUNIA - LEKULE

Breaking

21 Jul 2015

TANZIA: MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA DODOMA, MARIAM MFAKI AFARIKI DUNIA

MBUNGE wa Viti Maalum, Mariam Mfaki (CCM), amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa amelazwa.
Marehemu amekuwa mbunge kwa vipindi vitatu, 2010 - 2015, 2005 - 2010 na 2000 - 2005.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mohammed Mfaki amesema mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2012.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amen.






No comments: