Future kupiga show 4 Bure - LEKULE

Breaking

21 Jul 2015

Future kupiga show 4 Bure

Mkali mwenye sauti ya kipekee, mwenye uwezo wa Kurap na kuimba kupitia ukarasa wake wa instagram ametangaza kuwa atapiga show nne bure katika nchi ya marekani.
Show hiyo itafanywa kwenye miji tofauti ambayo ni Atlanta, Chicago, New York na Los Angeles ambapo nia ni kurudisha shukrani kwa mashabiki wake wanompa sapoti kwenye kazi yake ya muziki.

Future ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akitupiana maneno ya vijembe kwa aliyewahi kuwa mpenzi wake mwanadada Ciara, tayari ameaachia albamu yake inayoitwa Dirty Sprite 2 na pia atatumia show hizo za bure kwa nia ya kuitangaza kazi yake ya Dirty Sprity 2.




No comments: