MBUNGE
wa Jimbo la Mpanda Mjini, Bw. Said Amour Alfi (CHADEMA) ni miongoni
mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wamechukua na kurejesha
fomu za kuomba kugombea ubunge katika Jimbo jipya la Nsimbo, Wilaya ya
Mlele, mkoani Katavi kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa CCM mkoani Katavi, Averin Mushi
amethibitisha Bw. Arfi kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo
hilo.
Alisema
makada 23 wamejitokeza kuwania ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi
mkoani humo ambapo katika Jimbo la Nsimbo, makada ambao wamerejesha fomu
ni Bw. Arfi, Shabir Hasanali 'Dallah', Richard Mbogo, Manamba David na
Mapesa Frank.
Katika
Jimbo la Katavi ni Isaack Kamwelwe, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS), mkoani humo, Shafi Mpenda, Maganga Kampala na Osca Albano.
Kwa
upande wa Jimbo jipya la Kavuu, yupo Zumba Emmanuel, Mselem Abdalah
Said na Prudenciana Kikwembe ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu.
Jimbo
la Mpanda Mjini yuko Sebastian Kapufi, Galus Mgawe na Gabriel Mnyele na
Mpanda Vijijini ni Moshi Kakoso, Abdalah Sumry, Willy Makufe, Elizabeth
Sultan, Godfrey Nkuba, Rock Mgeju na Chifu Charles Malaki.
Mwenyekiti
wa CCM mkoani humo, Abdallah Mselem aliwaasa wanachama wa chama hicho
kujiepusha na wagombea wanaotumia ukabila, udini na hali yoyote ya
ubaguzi ili kupata uongozi.
"Wapo
wagombea wanaotumia misingi ya udini na ukabila kuwabagua wagombea
wenzao na kuwashawishi wanachama wasiwachague, kama mgombea yeyote
atabainika kufanya hivyo hatutamvumilia bali atashughulikiwa kwa mujibu
wa taratibu za chama," alisema.
No comments:
Post a Comment