Mteule
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya urais kwenye uchaguzi
mkuu ujao, Dk.John Pombe Magufuli, anaundiwa zengwe zito na wapinzani
wake kisiasa baada ya kubaini kuwa watapata taabu kubwa kuibuka na
ushindi katika patashika hiyo itakayofanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali, zengwe hilo linahusu kile kinachodaiwa
kuwa ni kuanza kwake mapema kufanya kampeni katika mikutano kadhaa
anayoifanya kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini, tangu alipoibuka
kidedea katika vikao vya mchujo ndani ya chama hicho tawala,
vilivyomalizika hivi karibuni mkoani Dodoma.
Akizungumzia
tuhuma hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema siyo
kweli kwamba mgombea wao ameanza kampeni mapema, bali kinachofanyika ni
utambulisho kwa wanachama wenzake wa CCM, ili wamtambue, kwa kuzingatia
kuwa ni mwenyekiti mtarajiwa wa chama hicho tawala.
Alisema
ni vigumu kwa mgombea huyo kupita mkoa wowote bila kwenda kwenye ofisi
ya chama kwa ajili ya kutambulishwa kabla ya kuanza kwa kampeni baadaye
mwezi ujao.
Akiwa
mkoani Mwanza wiki iliyopita, Dk. Magufuli alisema yupo njiani kwenda
nyumbani kwao Chato na kukanusha juu ya kufanya kampeni, kwani
kinachofanyika ni utambulisho na salamu tu.
No comments:
Post a Comment