Tungependa
kusahihisha propaganda nyepesi zinazoendelea kuenezwa ili kuusaidia
umma usiendelee kupotoshwa kwa mambo yasiyokuwa ya msingi huku kukiwa na
mambo makubwa yanayohitaji 'attention' ya Watanzania kuamua mustakabali
sahihi wa nchi yao kwa kuchagua MABADILIKO kupitia uchaguzi wa
kihistoria hapo Oktoba 25.
1. Zipo
taarifa zinaendelea kuenezwa kuhusu makada wa CCM wakiongozwa na Edward
Lowassa kuwa wana mpango wa kuhamia CHADEMA. Hadi sasa tunaziona habari
hizo kupitia mitandaoni na kwenye vyenye mainstream media. Bila shaka
wenye taarifa sahihi za mipango hiyo ni hao hao wanaozieneza. Nasi
hatuwajibiki kabisa kuwasaidia kutoa uhakika wa uenezi huo wanaofanya
kwa maslahi wanayoyajua.
2.
Viongozi wakuu wa chama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe
na Katibu Mkuu Dk. Willibroad Slaa wamekuwa wakiendelea na majukumu yao
mbalimbali kwa kadri ya nafasi zao na ratiba za chama hususan wakati
kama huu kuelekea defining moments za uchaguzi mkuu ambapo mara kadhaa
wamekuwa katika vikao na viongozi wakuu wenzao katika UKAWA ili kutafuta
mwelekeo sahihi kwenda Oktoba 25.
Wanaoeneza
habari kwamba Mkiti Mbowe na KM Dk. Slaa wamekuwa na mtafaruku eti kwa
sababu ya 'ujio dhanifu' wa Lowassa basi watu hao watakuwa hawajui
utaratibu wa utendaji kazi wa Chama kwa ujumla na hususan Viongozi hao
wawili ambao siku zote hufanya kazi kwa maelewano ya hali ya juu sana
kiasi cha kuendelea kuwa sehemu ya uimara wa CHADEMA.
3.
Propaganda hizo zinazojengwa katika misingi ya siasa nyepesi zimekwenda
mbali hadi kumsemea uongo mmoja wa waasisi wa CHADEMA Mzee Mtei eti
amekodiwa ndege kuja kutuliza mtafaruku.
3.
Tunajua lengo la upotoshwaji huo ni kutaka kuwachaganya Watanzania
wanaojiandaa kuiondoa CCM madarakani mwaka huu. Waenezaji uongo wanataka
kuwaaminisha Watanzania wanaowaka moto wa mabadiliko kuwa CHADEMA nayo
imegawanyika kama ilivyo kwa CCM ambayo imesambaratika juzi Dodoma kiasi
cha wajumbe kumzomea Mwenyekiti wao wa chama.
4.
CHADEMA iko imara kuliko wakati mwingine wowote ule, hasa katika kipindi
hiki ambapo inaendelea kujiandaa kuwatumikia Watanzania na kupanga
mikakati mbalimbali, kwa kushirikiana na washirika wenza kwenye UKAWA,
kuikabili CCM iliyomeguka vipande vipande na kuiondoa madarakani.
NB; Kuhusu #UKAWA Julai 14
Kama
ambavyo Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof. Ibrahim Haruna Lipumba alisema
Jumamosi usiku alipozungumza na waandishi wa habari kuwa leo umoja huo
utafikia na kutangaza kwa umma makubaliano juu ya mambo makubwa mawili;
1. Mgombea mmoja wa urais
2. Majimbo yaliyokuwa yamesalia katika mgawanyo kwa maana ya kusimamisha Mgombea mmoja
Aidha,
Prof. Lipumba alisema kuwa UKAWA wameshafanikiwa kufikia mwafaka katika
majimbo kwa asilimia 97 na sehemu iliyobakia ni ile ambayo itahitaji
mashauriano au (bilateral) mwafaka kati ya vyama viwili katika majimbo
fulani fulani ambapo vyama hivyo vilikuwa bado vinapitia vigezo
vilivyokubalika.
Tangu
asubuhi ya leo vikao vimekuwa vikiendelea. Majadiliano yamekwenda vizuri
kabisa. Baadae Summit (kikao cha Viongozi wakuu) itakutana kwa ajili ya
wayfoward na kuzungumza makubaliano kwa Vyombo vya Habari kwa ajili ya
Watanzania.
Vyombo
vya Habari vitataarifiwa muda na mahali ambapo Summit ya UKAWA itakutana
nao kwa ajili ya taarifa hiyo inayosubiriwa na umma wa Watanzania.
No comments:
Post a Comment