Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” katika pozi.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.

Siku moja
tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania kutangaza majimbo mapya ya
Uchaguzi,Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William
Bundala maarufu kwa jina la “Kijukuu cha Bibi K” ametangaza rasmi
kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la jipya
la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani
Shinyanga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Bundala
ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili
aweze kupeperusha bendara ya Chadema/UKAWA katika uchaguzi mkuu ujao
katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha
Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.
Mtia nia
huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge
katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo
hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama
anavyotakiwa Mbunge Kufanya.
Alisema
kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo
ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania maendeleo ya
wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na
watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za wilaya.
Sambamba
na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea
wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo
hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa
ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya
wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.
Aliongeza
kuwa akifanikiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo
jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la
saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la
ukosefu wa ajira kwa vijana.
Bundala
alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na
kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata
kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa Ardhi,Mirathi,haki
za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.
Akizungumzia
kuhusu suala la michezo katika jimbo hilo, Bundala alisema kuwa kupitia
Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa
michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi
kuu Tanzania Bara.
Awali
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu
Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana
mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge
wa jimbo hilo.
Wilaya ya
Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za Msalala,halmashauri
ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya
uchaguzi kuwa matatu.
Katika
kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi
ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA
wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.
No comments:
Post a Comment