Zoezi la uandikishwaji kwenye daftari la
kudumu la kupiga kura kwa njia ya kieletroniki BVR lipo mkoa wa Pwani
kwa sasa na linaanza rasmi leo tarehe 7 mwezi wa saba.
Zoezi hilo linatarajiwa kumalizika mnamo tarehe 20 ambapo uandikishwa utafanyika kwa awamu na makundi mawili.
Mratibu Uchaguzi mkoa wa Pwani ndugu
Shangwe Twamala ametoa ufafanuzi wa namna zoezi hilo litakavyofanyika
ambapo amesema, awamu ya kwanza itafanyika kwa siku saba kisha baada ya
hapo mashine zitahamishwa kwenda sehemu zilizosalia napo zoezi hilo
litafanyika kwa siku saba.
Pia Shangwe Twamala amewataka wakazi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi ili kufaniksha zoezi hilo.



No comments:
Post a Comment