Kazeti la Bild la nchini ujerumani
limeandika habari kwamba Kocha Mkuu wa Klabu bingwa wa kombe la
Bundesliga Bayern Munich, Pep Guardiola yupo radhi kubadilishana kwa
kuwatoa washambuliaji wake Thomas Muller na Arjen Robben na kiasi cha
fedha na kuwapa Manchester United ili wapewe winga machachari Angel Di
Maria.
Msimu uliopita Angel Di Maria hakuweza
kuonyesha cheche zake ndani ya Manchester United ambapo alitoka klabu ya
Real Madrid ya Hispania kwa ada ya paund million 60 lakini bado kocha
Pep amekua akimtolea macho Di Maria.
Hili linaweza kuwashawishi Manchester United ambao tayari walishaonyesha nia ya kutaka kusajili mshambuliaji Thomas Muller.



No comments:
Post a Comment