Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la
Biti Karo Mkazi wa Mkuranga, Kimanzichana Mtaa wa Makonde amefanya tukio
la ajabu na la kushanga kwa jamii, mara baada ya kukaa na mwili wa
marehemu Mama yake kwa muda wa siku sita ndani bila hata ndugu na
majirani zake kufahamu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kinasema Biti Karo alikuwa anakaa na Mama yake (Marehemu) akimuuguza.
Biti Karo aliyehusika kuuficha Mwili wa Marehemu
Chanzo chetu kinazidi kueleza kwamba, Majirani waliaanza kupata wasiwasi mara baada ya kutokumuona Mama huyo (Marehemu), kwani walikuwa wamemzoea akiwa nje na mwanae (Biti Karo) akiwa anampa dawa na chakula lakini ilipita siku kadhaa bila ya kumuona Mama huyo.
Majirani wakiwa kwenye eneo lililotokea msiba
Majirani walipoenda kumuulizia Biti Karo
aliwajibu kwamba hajambo na yupo ndani amelala, lakini mnamo tarehe 4
july kijana mmoja alihisi harufu kali sana maeneo ya nyumba ya Biti Karo
na alipojaribu kuuliza ni harufu ya nini, Biti Karo alijibu kwa kusema
kwamba inawezekana ni harufu ya Panya.
Mwili wa Marehemu ukionekana kwa mbali
Mnamo siku ya jumapili july 5 Mama mmoja
aliyejulikana kwa jina la Bibi Huruma ambaye ni ndugu wa Biti Karo
alikwenda kuwatembelea na kumjulia hali mgonjwa, alipofika alishangaa
kusikia harufu kali na alipouliza ni harufu ya kitu gani?, Biti Karo
hakujibu kitu chochote.
Bibi Huruma alipoingia ndani alikuta
Mama yao amefariki huku mwili wake ukitoa harufu na sehemu nyingine
zikiwa zimechanika na kupasuka ndipo hapo alipopiga mayowe na majirani
kusogea eneo hilo.
Majirani wote walishangaa kuona tukio
hilo ambapo wengine walienda kumtaarifu Mjumbe aliyejulikana kwa jina la
Kuisele, Mjumbe alimuita Mwenyekiti kisha wakawapigia simu Polisi.
Baada ya Polisi kufika na kuchukua maelezo waliamuru mwili wa marehemu kuzikwa.
Majirani wakiwa eneo la tukio
Chanzo chetu cha habari kinanaeleza
kwamba mwili wa marehemu ulikuwa umeharibika sana na ilikuwa ngumu hata
kuoshwa hivyo ulizikwa bila ya kuoshwa na wala kufanyiwa heshima yoyote.
Baada ya mwili wa marehemu kuzikwa Polisi waliondoka huku wakiwaacha wakazi wa eneo hilo kwenye hali ya kutofahamu nini kinaendelea kwani mpaka sasa Biti Karo yupo huru na wala haonyeshi hali ya kustushwa kwa kile kilichotokea.








No comments:
Post a Comment