Kampuni ya udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers
inapiga mnada wa nyumba ya mwanamuziki nyota wa bongo fleva, Lady Jay
Dee, baada ya kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya
EFC Tanzania Limited.
Kwa mujibu wa tangazo
lililotolewa jana katika moja ya magazeti ya kila siku, mnada huo
utafanyika saa 5:00 asubuhi kwenye eneo la kiwanja hicho lililopo
Mivumoni.
“Kwa idhini tuliyopewa na EFC Tanzania
Limited tutauza kwa mnada wa hadhara, dhamana/nyumba ya mdaiwa wa benki
hiyo,” linasema tangazo hilo.
“Mnada utafanyika tarehe
4/07/2015. Jina la mdaiwa/mdhamini- Judith Wambura Habash,
dhamana.nyumba itakayouzwa-Kiwanja Plot No. 54BLK4, Mivumoni Kinondoni
Dar es salaam, tarehe ya mnada-4/07/2015 kuanzia saa 5:00 asubuhi na
kuendelea,” linaongeza tangazo hilo.
Juhudi za kumpata
mwimbaji huyo wa kibao cha “Machozi” hakuweza kupatikana jana
kuzungumzia suala hilo, lakini Gadner Habash ambaye alikuwa na uhusiano
na Jay Dee na ambaye jina lake limeandikwa kwenye tangazo hilo kama jina
la tatu la mwanamuziki huyo, alisema hana taarifa hizo, hali kadhalika
meneja wake.
Habari kutoka ndani ya taasisi hiyo
zinasema kuwa mwanamuziki huyo alisitisha ghafla kulipa deni lake Juni
mwaka jana bila taarifa yoyote na hata alipokuwa akitafutwa, hakuwa
anapokea simu.
Kwa mujibu wa afisa kutoka kampuni ya
MEM, nyumba hiyo iliyotumika kama dhamana ya mkopo, ipo kwenye kiwanja
chenye ukubwa wa kilometa 901 za mraba, Tegeta Wazo na kina thamani ya
Sh40 milioni.
No comments:
Post a Comment