Lungi Maulanga alizwa na vibaka - LEKULE

Breaking

5 Jul 2015

Lungi Maulanga alizwa na vibaka

Msanii wa Bongo Movie nchini, Lungi Maulanga amejikuta akilizwa na vibaka baada ya kuibiwa baadhi ya vitu vya ndani wakati akiwa katika mtoko wa usiku hali ambayo imemtia hasara na kumrudisha nyuma kimaendeleo.
 
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo amedai kuwa tukio hilo lililotokea maeneo ya Magomeni, jijini Dar es Salaam limempa Lungi hasara kwani kitendo hicho ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
 

Lungi amekiri kulizwa na vibaka hao na kusema kuwa amechoka sasa kwani sio mara ya kwanza kufanyiwa kitendo kama hicho na kusema kuwa anajiandaa kuhama ili kukwepa adha hiyo na kudai kuwa ameibiwa vitu kadhaa ikiwemo Tv na deki.

No comments: