Chombo
cha NASA na taarifa zasayari za PlutoWana sayansi wa NASA kutoka
Marekani wanasema kuwa majaribio yao ya kurusha chombo kwenda katika
sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa.
Chombo
hicho kimefanikiwa kutuma taarifa katika kituo cha utafiti huo cha
Maryland zilizochukua takribani saa nne na nusu hadi kufika duniani na
kupokelewa na antenna NASA.
Saa
chache zijazo wanasayansi hawa wa NASA wameeleza kuwa wanatarajia kupata
mfululizo wa taariza zaidi na picha kutoka sayari hiyo ya Pluto ambazo
zitatoa uhalisia wa undani wa sayari hiyo ya Pluto.



No comments:
Post a Comment