Zanzibar.
Wanafunzi 38,853 wamefaulu mitihani yao ya kidato cha sita kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mtihani huo mwaka huu, huku matokeo yakionyesha kuwa shule za Serikali na binafsi zimeenda sambamba.
Wanafunzi 38,853 wamefaulu mitihani yao ya kidato cha sita kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mtihani huo mwaka huu, huku matokeo yakionyesha kuwa shule za Serikali na binafsi zimeenda sambamba.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) jana, wanafunzi 35
walishindwa kufanya mitihani hiyo baada ya kuugua ghafla.
Akitangaza
matokeo hayo mjini Zanzibar jana, katibu mtendaji wa Necta, Charles
Msonde alisema kati ya wahitimu waliofaulu, wasichana ni 11,734, sawa na
asilimia 98.56 na wavulana ni 27,119, sawa na asilimia 97 ya
watahiniwa.
Kwa mujibu wa Msonde, Shule ya Sekondari ya
Feza ya jijini Dar es Salaam iliongoza katika orodha ya shule 10 bora
inayojumuisha pia shule za Runzewe (Geita), Feza Girls (Dar), Sumbawanga
(Rukwa), Ivumwe (Geita), St Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Vwawa (Mbeya),
Kisimiri (Arusha), Namabengo (Ruvuma) na Scolastica (Kilimanjaro).
Orodha
ya shule kumi zilizofanya vibaya inaongozwa na Shule ya Sekondari ya
Meta ya Mbeya, iliyoshika mkia ikifuatiwa na Kwiro (Morogoro), Mtwara
Tech (Mtwara), Iwalanje (Mbeya), Lugoba (Pwani), Kaliua (Tabora),
Kilangalanga (Pwani), Lwangwa (Mbeya), Ilongero (Singida) na Bariadi ya
Simiyu.
Msonde alisema kwamba kiwango cha ufaulu kwa
matokeo ya kidato cha sita kimekuwa kikiongezeka kila mwaka kutokana na
juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuboresha kiwango cha
elimu kwa maendeleo ya Taifa na wananchi wake.
Alisema
kwamba matokeo ya mtihani ya mwaka huu yanaonyesha kiwango cha ufaulu
kimepanda kwa asilimia 0.61 kutoka asilimia 98.26 mwaka 2014 hadi
asilimia 98.87 mwaka 2015.
Alisema kwamba katika shule
kumi bora kitaifa, kuna shule tano za Serikali wakati katika orodha ya
shule 20 bora, shule 13 za Serikali zimeongoza, zikifuatiwa na shule
saba za binafsi.
Hata hivyo, alisema wanafunzi 35
walishindwa kufanya mitihani yao, wakiwamo 10 ambao walishindwa kumaliza
mitihani baada ya kuugua na 25 waliougua kabla ya mitihani kuanza na
kwamba Necta imeafiki wanafunzi hao warudie mitihani yao Mei mwakani.
“Kati
ya wanafunzi hao watano wamefutiwa matokeo ya mitihani baada ya
kuthibitika waliingia kwenye vyumba vya mtihani wakiwa na karatasi za
kuwasaidia kujibu maswali ya mitihani wakati ni kinyume na sheria,”
alisema Msonde.
“Watahiniwa waliofanya vizuri zaidi
wamepatikana kwa kulinganisha wastani wa pointi kwenye masomo ya
tahasusi pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata katika masomo
yao,” alisema Msonde.
Msonde alisema kwamba wanafunzi
hao wameonyesha uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi na kuingia katika
kundi la wanafunzi wenye kipaji maalum wa mchepuo wakitoka katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara.
Aliwataja wanafunzi kumi
bora kitaifa waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kuwa ni
Ramadhani Gembe (Feza Boys), Lesian Lengare (Ilboru), Hunayza S Mohamed
(Feza Girls), Riosemary Osian Chengula (St Mary’s Mazinde Juu), Kevin
Fidelis Rutahoile (St Joseph Cathedral), Anderton A Masanja (St Joseph
Cathedral) Joseph Pasia (Ilboro) Lupyana Kinyamagoha (Mzumbe), Yonazi
Charles Senkondo (Feza Boys) na Meghna Solanki kutoka Shule ya Shaaban
Robert.
Aliwataja wasichana kumi bora wa kitaifa
waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kuwa ni Hunayz S Mohamed
(Feza Girls), Rosemary Osian Chegula (St Mary’s Mazinde Juu), Meghna
Vipul Solanki (Shaaban Robert), Nice Robert Mathew (St Mary’s Mazinde
Juu), Atumpoki Francis Mwakyoma (St Mary’s Mazinde Juu), Irene Godlove
(Feza Girls), Kuduishe Kisowile (St Mary’s Mazinde Juu), Aziza Ramadhan
Mkwizu (St Mary’s Mazinde Juu), Zaituni Rashid Langi (Iringa Girls
pamoja na Fatma Moshi (Feza Girls).
Upande wa wavulana
waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi ni, Ramadhan Gembe, (Feza
Boys), Lesian Lengare (Ilboru), Kevin Fidelis Rutahoile, Anderton
Masanja, Joseph Pasian, Lupyana Kinyamagoha (Mzumbe), Yonazi Charles
Senkondo (Feza Boys), Erickson Muyungi (Nyegezi Seminary), Malonja Yona
(Ilboru) na Amani Pelesi Fungo kutoka Feza.
Kwa mujibu
wa matokeo hayo, Shule za Zanzibar zimeshindwa kuingia miongoni mwa
shule zilizotoa watahiniwa kumi bora kitaifa pamoja na shule kumi bora
zilizofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita iliyofanyika Mei
mwaka huu.
Katibu huyo mtendaji aliwatangaza wanafunzi
bora wa masomo ya biashara, lugha na sanaa pamoja na matokeo ya
mitihani ya ualimu iliyofanyika mwaka huu



No comments:
Post a Comment