Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wamekamilisha mpango wa kumsajili kiungo kutoka nchini Brazil na klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine, Douglas Costa.
Miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani imekamilisha dili hilo baada ya kutoa kiasi cha ada ya uhamisho wa paund million 21.3 ambazo ni sawa na Euro million 30.
Mbali na kukamilisha mpango wa fedha za usajili, pia The Bavarians wamemsainisha mkataba wa miaka mitano Costa, ambao utamuwezesha kukaa Allianz Arena mpaka mwaka 2020.
Huko nchini Ukraine taarifa zinaeleza kwamba, uongozi wa kklabu ya Shakhtar Donetsk nao umethibitisha taarifa za kuondoka kwa Douglas Costa mwenye umri wa miaka 24, na wamemtakia kila la kheri katika maisha yake mapya huko nchini Ujerumani.

No comments:
Post a Comment