FC Porto Wamalizana na Atletico Madrid - LEKULE

Breaking

1 Jul 2015

FC Porto Wamalizana na Atletico Madrid

Hatime uongozi wa FC Porto, umethibitisha taarifa za mshambuliaji kutoka nchini Colombia Jackson Martinez, kujiunga na klabu ya Atletico Madrid baada ya kukamilishwa kwa taratibu za uhamisho wa paund million 24.8.
FC Porto wamethibitisha taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji huyo kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa kukiri kukutana na viongozi wa Atletico na kumaliza mipango yote ya uhamisho.

Martinez mwenye umri wa miaka 28 anaondoka nchini Ureno huku akiacha kumbu kumbu kwa mashabiki wa soka nchini humo, baada ya kuwa kinara wa upachikaji wa mabao msimu uliopita.

No comments: