Watanzania wameonywa kuwa makini kwa kutokubali kuvurugwa na watu
wanaotangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka
huu, badala yake wafanye maamuzi sahihi kwa kumchagua kiongozi
atakayekuwa tayari kulinda rasilimali za nchi na asiye mpenda rushwa.
Kauli hiyo imetolewa na Benard Membe wakati akitafuta wadhamini
mkoani Ruvuma ambapo wanachama zaidi ya elfu tano walijitokeza
kumdhamini.
Aidha aliwaomba wananchi wachague mtu ambaye atakuwa na uzalendo wa
nchi na ambaye atalinda rasilimali za nchi na kusimamiapia asiwe
penda rushwa.
Mgombea huyo amesema ,iwapo wataridhika kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa
kuongeza watanzania zaidi ya milioni 45 hawana budi kumchangua.
Katika hatua nyingine mgombea nafasi ya uraisi makongoro Nyerere pia
aliwataka watanzania kuwa makini na wagombea na wawasikilize na badaye
wachague mtu ambaye ataweza kulinda chama na masirahi ya watanzania
No comments:
Post a Comment