BIG SEAN AJA NA STUDIO,AIPA SHAVU SHULE YAKE - LEKULE

Breaking

12 Jun 2015

BIG SEAN AJA NA STUDIO,AIPA SHAVU SHULE YAKE


Ukizungumzia marapa wanaodumu kwenda na style ya michano ya kisasa huwezi kukosa kumtaja rapa Big Sean kijana mtanashati aliyewahi kutoka kimapenzi na mwanadada Ariana Grande.
Rapa huyo baada ya kuanza kupata mafanikio, hatimaye ameanza kurudisha kile anachokipata kwa jamii yake inayomzunguuka.

Kwa kuanza, Big Sean akisaidiwa na kampuni ya vifaa vya michezo adidas amefungua studio ya kurekodi nyimbo, katika eneo la shule aliyowahi kusoma Cass Tech huko nchini Marekani.
Studio hiyo inayoitwa “Sean Anderson Studio” licha ya kuwa na lengo la kuwasaidia wanafunzi na wasanii wa eneo hilo lakini pia atakua anaitumia kwa kazi zake.

Kwenye picha aliyotupia katika akaunti yake ya instagram,Big Sean aliandika “Siwezi kuamini, nilikuwa narap katika meza za chakula za hapa shule,

ilikuwa shida kurekodi, lakini kwa kipindi kisichozidi miaka 10 nimewafanikiwa kufungua studio yangu, hii inasababisha nilie kwa furaha”.

No comments: