BANGI YAMTIA PINGU RICK ROSS - LEKULE

Breaking

12 Jun 2015

BANGI YAMTIA PINGU RICK ROSS


Jumatano ya wiki hii, rapa mwenye mwili mkubwa anayejulikana kwa jina la Rick Ross a/k/a Rozay alijikuta mikononi mwa poli wa mji wa Atlanta baada ya kudakwa akivuta bangi ndani ya gari lake.

Wakati Rose akiendelea na safari yake mitaa ya Fayette Country, Georgia alijikuta akisimamishwa na polisi wa usalama barabarani ambapo walitaka kukagua kama gari lake lipo salama kwa kuendeshwa.

Baada ya kufika eneo hilo na kuongea na Rapa huyu, polisi waligundua kwamba jamaa anatoa harufu ya bangi ndipo hapo walipo amuakwenda nae kituoni kwa maaelezo zaidi.

Kwa Rozay hii itakua mara ya pili kukumbwa na mkasa wa kukamatwa na bangi.

No comments: