MESSI APEWA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA NNE - LEKULE

Breaking

12 Jun 2015

MESSI APEWA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA NNE


Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona, Lionel Andrés “Leo” Messi Cuccittini anatajwa kuwa katika morari kubwa ya kuwaongoza wachezaji wenzake wa timu ya taifa wakati wa fainali za mataifa ya kusini mwa Amerika (Copa America) zitakazoanza kutimua vumbi lake Juni 12 nchini Chile.

Messi ametajwa kuwa katika hali hiyo, kufuatia upepo mzuri kupita katika klabu yake msimu wa 2014-15 ambapo ilishuhudiwa wakitwaa mataji matatu huku yeye akionekana kuwa mstari wa mbele katika upatikanaji wa mafanikio hayo.

Wadadisi wa soka duniani amesema Messi anakwenda kuongeza chachu ya kusaka mafanikio mengine kwa mwaka huu akiwa na timu yake ya taifa, huku wachezaji wenzake wakitamani kufanya makubwa kama ilivyokua kwa mchezaji huyo.

Jambo lingine ambalo linatajwa kuchagiza hamasa katika kikosi cha Argentina, ni hatua ya timu hiyo kufika kwenye mchezo wa fainali wa kombe la dunia mwaka 2014 na kufungwa bao moja kwa sifuri na timu ya taifa ya Ujerumani.

Hatua hiyo inatazamwa kama mtihani kwa wachezaji wa Argentina ambao hawatotaka kuonyesha kushindwa tena kwenye michuano mikubwa duniani kama ya Copa America.

Tayari Lionel Messi ameshajiunga na wachezaji wenzake kambini na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina ambacho kitacheza mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya Copa America Juni 13, dhidi ya Paraguay.

Argentina wamepangwa katika kundi la pili sambamba na Jamaica, Paraguay na Uruguay.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya taifa ya Uruguay.

No comments: