Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevitahadharisha vyama vya siasa kuzingatia Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati mchakato wa kutafuta wagombea ukiendelea.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevitahadharisha vyama vya siasa kuzingatia Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati mchakato wa kutafuta wagombea ukiendelea.
Mutungi alionya kuwa mwanasiasa yeyote atakayekiuka sheria hiyo atawekewa pingamizi wakati wa uteuzi ndani au nje ya chama.
Alisema
ofisi yake itachukua hatua dhidi ya ukiukwaji wa sheria hiyo kama
itajiridhisha na ushahidi utakaotolewa. Hata hivyo, alisema hawezi
kuzungumzia mchakato wa kutangaza nia unaoendelea sasa kwa sababu bado
wanafuatilia mwenendo wa wanasiasa.
“Ofisi yangu ni mwangalizi na msimamizi wa sheria hii, kwa hiyo tuna jukumu la kuhakikisha sheria inafuatwa,”alisema.
Kifungu
cha 24 (2) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi, kinasema mgombea yeyote,
au wakala wake, au chama chake kikihusika kuvunja masharti yaliyotajwa
katika sheria hiyo basi mgombea huyo au chama kitaondolewa katika hatua
ya uteuzi au uchaguzi.
Msajili Msaidizi, Kitengo cha
Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma, Piencia Kiure alisema Kifungu cha
14 cha Sheria hiyo kinasema gharama zote za wagombea zitabebwa na chama
husika. “Sheria inataka chama kutumia chini ya Sh2 bilioni ngazi ya
rais na majimbo gharama italingana na ukubwa na idadi ya watu katika
jimbo husika,” alisema Kiure.
No comments:
Post a Comment